MABADILIKO YA TAREHE YA KUFUNGUA SHULE
Ndugu
mzazi salamu,
YAH: MABADILIKO
YA TAREHE YA KUFUNGUA SHULE
Leo
tarehe 02/09/2022 Shule imepokea taarifa ya mabadiliko ya tarehe ya kufungua
shule kutoka kwa OR-TAMISEMI Kuwa Tanzania
imepewa heshima ya kuwa mwenyeji wa mashindano ya wanafunzi wa Jumuiya ya
Afrika Mashariki na kati (FEASSA).
Mashindano hayo yatafanyika katika mkoa wa Arusha. Miongoni mwa taasisi
zilizochaguliwa kuwapa malazi wanamichezo ni shule yetu ya TRUST ST PATRICK.
Hivyo basi, shule zitafunguliwa kama ifuatavyo:-
1. Wanafunzi wote wa bweni
kuanzia chekechea mpaka darasa la sita wataripoti shuleni tarehe 25/09/2022.
2. Wanafunzi wote wa kutwa(day)
kuanzia chekechea mpaka darasa la sita wataripoti tarehe 26/09/2022.
3. Likizo ya nusu muhula iliyotakiwa
kuanza tarehe 30/09/2022 hadi tarehe
10/10/2022 HAITAKUWEPO ili kufidia
siku ambazo zimetumika kwa michezo.
Shule
itakapofunguliwa tarehe 26/09/2022 haitafungwa mpaka tarehe 08/12/2022