MASHINDANO YA MICHEZO YA SHULE ZA AFRIKA MASHARIKI (FEASSSA) YATAKAYOFANYIKA MWEZI SEPTEMBA, 2022.
YAH: MASHINDANO YA
MICHEZO YA SHULE ZA AFRIKA
MASHARIKI (FEASSSA)
YATAKAYOFANYIKA MWEZI SEPTEMBA, 2022.
Tafadhali
husika na mada tajwa hapo juu
2.
Mashindano ya Michezo yanayohusisha wanamichezo kutoka nchi
wanachama
wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (FEASSSA) yatafanyika Mkoani
Arusha
kuanzia tarehe 10-24 Septemba, 2022.
3.
Mashindano haya yatahusisha Wanamichezo zaidi ya elfu nne (4000) kutoka
katika
nchi hizo.
4.
li kufanikisha mashindano haya muhimu, unaombwa kushiriki kikamilifu katika
maandalizi
ya mapokezi ya wageni wa mashindano haya ikiwa ni pamoja na Shule
yako
kutumika kama Kituo cha kulaza wanamichezo tarajiwa.
5. Kutokana na Shule yako kuwa kituo cha kulaza
Wanamichezo hao,
utalazimika kufunga Shule kwa muda huo hadi Michezo
itakapomalizika,
isipokuwa kwa Madarasa ya Mitihani ya Taifa. Aidha Shule husika
zitafunguliwa tarehe 26/09/2022. Siku zilizotumika wakati wa
FEASSSA zifidiwe
wakati wa likizo ya mwezi Disemba, 2022.
6.
Waraka wa Elimu Na.1 na 2 wa Mwaka 2022 kuhusu Kalenda ya Mihula ya
masomo
kwa Shule za Awali, Msingi, Sekondari pamoja na kidato cha Tano na Sita
umeambatishwa
kwa rejea.